
Ni swali zuri unaloweza kujiuliza, lenye jibu rahisi kuliko unavyoweza kutegemea, kimsingi Fid Q na Joh Makini ni wasanii ambao uzito wao hautofautiani sana, lakini ukiwapambanisha, ni Joh Makini, ndo atakaye ibuka na ushindi, unajua sababu ni nini? . Joh Makini anaumiza sana kichwa, anacho kiimba ni kile anacho kifikiria yeye mwenyewe, i mean anaimba mawazo yako mwenyewe( independent thinking ). Wakati Joh Makini akifanya hivyo, Ngosha yuko busy kwenye library yake akisoma vitabu na majarida ya aina mbalimbali, huku akitazama movies pia. Unajua kinachofuatia ni kitu gani?, ana chukua jumbe anazozisoma kwenye vitabu hivyo, au scripts za kwenye movies na kuziimba kana kwamba ni za kwake mwenyewe( plagiarism), anacho kifanya ni kubadili lugha kutoka kwenye kiinegreza kwenda kwenye kiswahili ( huu ni uharamia wa kitaaluma ). Anacho kifanya Fid Q ni hatari sana dhidi ya maendeleo ya muziki wake mwenyewe kwa sababu kwanza, anacho kiimba watu wa kawaida( wasio enda shule ), wanakuwa hawakielewi huku walio enda shule wanakuwa wanmchora tu na kumuona zaidi kama mtafisiri kuliko msanii kichwa anaye fikiri.Tatizo hili analo pia Mwana FA( Nitalizungumzia kwa undani zaidi siku za mbeleni ). Kwa mtindo huo, wasanii wa kaliba ya Joh Makini, Nako 2 Nako,Chid Benz, Mansu Li,kwa kuwataja wachache wataendelea kuheshimika sana katika tasnia ya muziki wa hiphop ya bongo ndani na nje ya bongo, kwa nini? kwa sababu wanaumiza vichwa, hawaandiki mistari ya tafsiri. Kwa mfano Nako 2 Nako, huwa hawaimbi filosofi, wao wanaimba juu ya mambo ya kawaida kabis yanayotokea mitaani, tena kwa lugha rahisi inayoelewa, ndio maana wanaheshimika na kukubalika sana, katika jamii ya mashabiki wa muziki wa hiphope. Msanii wa hiphope anapotumia lugha ya kawaida na mawazo ya kawaida ndivyo anavyoweza kuwateka mashabiki. Kwa mfano ,hebu msikilize Fid Q kwenye track ya "Usinikubali Haraka"; Ni traki ya ukweli sana na imewashika sana mashabiki wa muziki kwa sababu ametumia lugha ya kawaida sana. Ninaamini Fid Q anao uwezo mkubwa sana wa kuandika masahiri mazuri bila kutumia mawazo ya watu wengine, traki kama "Huyu na Yule" ni mfano mzuri wa kazi zake alizo fanya kwa kutumia mawazo yake mwenyewe. Hii ni changamoto kwa wasanii wa hiphope wa kaliba ya Fid Q na Mwana FA.

No comments:
Post a Comment