Saturday, October 10, 2009

HABARI NJEMA KWA WASANII WA AINA ZOTE ZA SANAA NCHINI TANZANIA.

Kwa mara ya kwanza kabisa, nchini Tanzania, kampuni inayojishughulisha na utunzaji wa kumbukumbu za aina zote kwa njia ya maandishi,sauti,picha,video na intaneti inayokwenda kwa jina la; tanPEDIA, inakuletea THE ENCYCLOPAEDIA OF ALL TANZANIA ARTISTS.( AN ALL TANZANIAN ARTISTS DIRECTORY ) Ni juzuu ama kitabu kikubwa chenye mkusanyiko wa taarifa na kumbukumbu za pamoja za wsanii wa aina zote za sanaa nchini Tanzania kuanzia muziki wa kila aina, maigizo, filamu, usui, uchongaji, uchoraji, sarakasi,mazingaombwe nakadhalika. Encyclopaedia hiyo itajumuisha wasanii wa aina zote za sanaa wenye majina na wasio na majina( undergrounds),waliopo hai na walio tangulia mbele za haki, waliopo ndani na nje ya Tanzania.

Ikiisha kamilika, encyclopaedia hii itasambazwa katika maktaba zote za taifa zilizopo katika mikoa yoye nchini,maktaba za mashule,taasisi,vyuo na vyuo vikuu vyote nchini Tanzania na katika nchi za jirani, pamoja na majumba yote ya makumbusho nchini na katika nchi za jirani, vilevile encyclopaedia hiyo itawekwa online( mtandaoni). Dhumuni la kuandaa encyclopaedia hiyo ni kuwatangaza kibiashara wasanii wa aina zote za sanaa wa kitanzania kitaifa na kimataifa, ikiwa ni pamoja na kutunza kumbukumbu zao kwa ajili ya vizazi vijavyo. Kwa wewe msanii wa aina yoyote ya sanaa wa kitanzania uliye ndani au nje ya nchi ambaye unataka taarifa na kumbukumbu zako zijumuishwe katika encyclopaedia hii, unatakiwa kulipia REGISTRATION FEES, ambayo ni kiasi cha shilingi za kitanzania ELFU ISHIRINI NA TANO TU( THS 25,000/=). Kauli mbiu yetu ni VOX AUDITA PERIL LITERAL SCRIPTA MANET! au kwa kiingereza SPOKEN WORDS PERISH, BUT WRITEN WORDS SURVIVES! kwa kiswahili MANENO YA KUTAMKWA HUTOWEKA, LAKINI MANENO YALIYO HIFADHIWA KATIKA MAANDISHI HUDUMU!
Kwa maelezo zaidi watembelee katika blog yao: http/www.tanpedia.blogspot.com/ ama waandikie; tanpedia@gmail.com.

No comments:

Post a Comment