Thursday, October 8, 2009

KUFURU ZA REMMY MA, NDO ZILIZO MPELEKA GEREZANI!


Mdau unaikumbuka albamu ya Remmy Ma, aliyoibatiza jina la SHESUS KHRIST?, Unalikumbuka cover la albam hiyo?, God Forbid! How blasphemy is that?. Albamu hiyo na cover la albamu hiyo ndo vinavyo elezwa kuwa chanzo cha mdada huyo kutupwa gerezani miaka kitatu kwa kosa la kumshambulia mdada mwenzake kwa risasi na kumsababishia ulemavu kwenye club moja ya usiku, akimtuhumu kumuibia dola 3000 zilizokuwa kwenye pochi yake ( was she high or something?, i bet she was high). Tangu Remmy ma atoe albamu hiyo,amekuwa akiandamwa na matukio ya ajabu na amekuwa akifanya mambo kama mtu aliyechanganyikiwa hivi( cocaine or something? sijui!!),jambo linalo tafsiriwa kama laana kutoka kwa Mungu. Mfano katika tukio la kustaajabisha, Remmy Ma, bila ya wasiwasi wowote, aliperform jukwaani huku viungo vyake vya uzazi vikiwa vinaonekana. ( Damn!, this is not hiphope!).
Vituko vya wasanii wa kariba ya Remmy Ma, ambao sisiti kuwaita mamluki wa hiphope ndo vinavyo ufanya muziki wa hiphope upoteze uthamani wake na kuonekana kama muziki wa wahuni, jambo ambalo si la ukweli hata kidogo. Anyway MAMAHIPHOPE MAGAZINE tunamuombea Mungu our SISTER-IN-HIPHOPE, aweze kutumikia kifungo chake salama, na atoke akiwa amebadilika kitabia, ajutie makosa yake, atubu na marudie Mungu wake. Sisi tumekwisha msamehe na tuna ahidi kumpokea kwa mikono yote miwili siku atakayo bisha hodi kwa mara nyingine kwenye hili game la hphope.

No comments:

Post a Comment