Wednesday, October 14, 2009

JOHN SINGLETON NA WATU WEUSI.


Akimtumia mhusika Tupac Amaru Shakur,katika movie ya POETIC JUSTICE Mwandishi na muongozaji mahiri wa filamu nchini Marekani,John Singleton anamuelezea mtu mweusi katika namna tofauti tofauti. John Singleton anawaelezea watu weusi kama watu wasio na staha, wasio wastaarabu( watu wasio weza kuishi kwa kufuata utaratibu), wasioweza kukaa pamoja kwa amani ( bila kugombana kwa sababu zisizo na msingi), n.k. Picha lenyewe lilikuwa hivi;vijana wanne ( wasichana wawili na wavulana wawili), waliukuwa wakisafiri kutoka Los Angeles California kwenda San Francisco kwa ajili ya mapumziko mafupi. Baada ya mwendo mrefu, walifika katika eneo moja la wazi mfano wa bustani. Ni harufu ya vyakula vizuri ndo iliyo wastua vijana haio ambao kwa muda huo walikuwa na njaa ya kutosha. Waliposhuka kwenye gari macho yao yalikumbatiwa na umati mkubwa watu ( wote weusi ) waliokuwa wakifanya mambo tofauti tofauti ikiwa ni pamoja na BERBAQUE. Kwa ifupi ilikuwa ni FAMILY REUNION. Wakiwa wanashangaa mmoja kati ya watu waliokuwa katika sherehe hiyo aliwakaribisha wa bashasha akimuita Tupac Shakur , " cousin", naye akishajua kuwa jamaa hana uhakika na anachokifanya akaitikia na kuaribishwa yeye pamoja na wenzake. Mambo mengi yalitokea hapo. Tupac Shakur na Janet Jackson wakiwa wanapata msosi( walikuwa wameshakaa kwenye eneo hilo kwa takribani dajika 20 hivi au zaidi) , ndipo Mwandishi John Singleton akimtumia Tupac Shakur anamuelezea mtu mweusi katika namna ifuatayo;

" Since i have born, i have neva seen a large group of black people like this one, and there are no some fightings".


Mdau, unatafsiri hivi sentensi hiyo?

No comments:

Post a Comment